Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mh. Paul Makonda amefunguka na kuwaomba msamaha baadhi ya wananchi ambao ameshindwa kutimiza ndoto zake na kusema anaamini ataendelea kuwatumikia na kujitahidi kuweza kugusa maisha ya kila mmoja.
Paul
Makonda amesema hayo siku mbili baada ya kutimiza miaka miwili toka
ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kusema kuwa ndani ya
miaka miwili akiwepo madarakani anaamini amegusa maisha ya watu kwa
kutumia kipaji chake, uwezo wake wote.
"Asante Mungu kwa neema zako, kama usingekuwa upande
wangu na Dunia iseme sasa. Nawashukuru sana sana watumishi wenzangu Kwa
kunivumilia na kunielewa katika kutimiza majukumu yangu. Zaidi
nawashukuru sana wananchi naimani nimejitahidi kuwatumikia Kwa moyo
wangu wote na vipaji vyote na pale niliposhindwa kutimiza ndoto yenu
mnisamee"
Makonda aliendelea kufafanua na kutoa ahadi yake kwa wananchi kuwa
"Zaidi nawaahidi nitaendelea kujituma zaidi ili niyaguse
maisha ya kila mmoja wetu kama ambavyo Serikali ya awamu ya 5
inavyokusudia. Mwisho si kwa umuhimu ni Kwa wadau wa maendeleo naomba
mfahamu kila cent mliyoitowa ina thamani kwangu na kwa wananchi wangu.
Tumefanya Mambo mengi na hakika na tumegusa na hata kuleta faraja Katika
maisha ya Watu wengi. Kwakutambua mchango wenu ninaandaa siku ya
kuwatambua na kuwatunuku tuzo kama asante yangu kwenu"
Machi 13, 2016 Paul Makonda aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam
Post A Comment: