Mzunguko wa 22 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaendelea wikiendi hii Machi 11, 2018 kwa kuchezwa mechi tano (5).
Mechi mbili za mzunguko huo zilizokuwa zichezwe Machi 11, 2018 zimebadilishiwa Simba SC waliokuwa wacheze ugenini dhidi ya Njombe Mji mchezo huo sasa utapangiwa tarehe nyingine baada ya wekundu hao wa Msimbazi kuomba kusogezwa mbele ili kupata muda wa maandalizi yao ya marudiano dhidi ya Al Masry Kombe la Shirikisho utakaochezwa Port Said nchini Misri Machi 17, 2018.
Mchezo wa Kagera na Mwadui uliokuwa uchezwe Machi 11, 2018 kwenye Uwanja wa Kaitaba sasa utachezwa Jumanne Machi 13, 2018 kutokana na kusogezwa kwa mechi yao dhidi ya Young Africans uliyochezwa jana Machi 9, 2018.
Mechi nyingine za mzunguko wa 22 zitakazochezwa Jumapili Machi 11, 2018
AzamFC vs Mbao FC (Azam Complex,Chamazi)
Ruvu Shooting vs Mbeya City (Mabatini)
Singida United vs Ndanda (Namfua)
Majimaji vs Lipuli (Majimaji)
Tanzania Prisons vs Mtibwa Sugar (Sokoine)
Post A Comment: