Usiku wa kuamkia leo Jumapili Machi 04, 2018 mtu mmoja ambaye jina lake halijatambulika hadi sasa amejijiua kwa kujipiga risasi nje ya Ikulu ya Marekani mjini Washington.
Tokeo la picha la white house man kills himself
Jengo la White House
Kwa mujibu wa Mtandao wa Shirika la Habari la ABC umeripoti kuwa mtu huyo alikuwa karibu na geti la White House na alianza kufyatua risasi akielekeza Ikulu na kisha baadae kujipiga risasi mwenyewe.
Tokeo la picha la white house man kills himself
Hata hivyo, Rais wa Marekani Donald Trump na Familia yake hawakuwepo Ikulu wakati wa tukio hilo likitokea walikuwa mjini Florida ambako imeelezwa walienda kupata chakula cha usiku.
Tokeo la picha la white house man kills himself
Mashuhuda waliyokuwepo kwenye tukio hilo waliohojiwa na gazeti la Washington Post wamesema kuwa mtu huyo alikuwa kwenye msongamano wa watu na alizua taharuki baada ya kufyatua risasi.
Jeshi la Polisi mjini Washington tayari limetoa taarifa juu ya tukio hilo ambapo limedai kuwa mtu huyo amefariki dunia na hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa huku likikiri wazi kuwa jina la mtu huyo bado halijatambulika na uchunguzi unaendelea.

Rais Trump hadi sasa bado hajatoa tamko lolote hadi sasa ingawaje watalaamu wa Masuala ya Kidiplomasia na Siasa wanahusisha tukio hilo na mambo yanayoendelea ndani ya Ikulu ya Marekani.
Wiki iliyopita baadhi ya watumishi White House walijiuzulu kuhudumu baada ya kudai kuwa majukumu yao yanaingiliwa na mtoto wa kike wa Trump, Ivanka Trump na mumewe .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: