Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida  Miraji Mtaturu akiwa  na mtendaji wa mahakama mkoa, mkurugenzi wa halmashauri hiyo pamoja na maafisa ardhi wilaya katika kikao cha pamoja kilichofanyika ofisini kwake.
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu akizungumza na mtendaji wa mahakama mkoa, mkurugenzi wa halmashauri na maafisa ardhi katika kikao cha pamoja ofisini kwake.
 Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi wakiwa katika kikao na mkuu wa wilaya hiyo mh Miraji Mtaturu hayupo pichani.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida  Miraji Mtaturu akiwa ofisini kwake katika kikao cha pamoja na mtendaji wa mahakama mkoa, mkurugenzi wa halmashauri na maafisa ardhi ambao hawapo pichani.


Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida  Miraji Mtaturu ametoa mwezi mmoja kwa halmashauri hiyo kuhakikisha wanaandaa maeneo na hati kwa ajili ya ujenzi wa mahakama za mwanzo kwa kila kata.

Mahakama hizo zitajengwa katika kata zote 28 zilizopo wilayani humo sambamba na mahakama ya wilaya.

 Mtaturu ametoa agizo hilo ofisini kwake alipokutana na mtendaji wa mahakama mkoa, mkurugenzi wa halmashauri na maafisa ardhi wilaya kwa lengo la  kujadili kuhusu  upatikanaji wa viwanja na hati kwa ajili ya kujenga mahakama hizo.

Akizungumza katika kikao hicho Mtaturu amesema mpango wa wilaya ni kujenga mahakama za mwanzo katika kata zote 28 zilizopo wilayani humo.

"Wilaya yetu ina jumla ya kata 28, mpango wetu ni kuwa na mahakama za mwanzo katika kata zote na kuwa na mahakama ya wilaya ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi,"alisema  Mtaturu.

Amesema wanaposimamia utawala bora wanapaswa kwenda sambamba na kuweka mazingira rafiki ya utoaji haki na hiyo itakuwa ni namna moja ya kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli ambaye katika uongozi wake anahakikisha anawatetea wanyonge.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: