Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC, Dismas Ten amewaambia mashabiki wa timu hiyo kuacha kulaumu na kuwafundisha viongozi chakufanya bali waje uwanjani kuunga mkono timu zao.
Ten ameyasema hayo leo kwenye mkutano na wanahabari muda mchache kabla ya uzinduzi wa masuala ya kidijitali ya klabu hiyo, ambayo yatatoa huduma ya taarifa mbalimbali zinazohusu timu hiyo kwa mashabiki wake.
''Tunao mashabiki wengi kwasasa wamekuwa wakizungumza vitu vingi, kusema watu, kutukana watu ni wakati sasa wakuacha kufanya hivyo badala yake wajitokeze uwanjani kutoa nguvu ya 12 kusapoti wachezaji'', amesema Ten.

Ten pia amefafanua kuwa watu wengi walikuwa wanamuuliza kwanini hajaenda na timu Botswana ambapo amesema Yanga ni taasisi kubwa na ina wafanyakazi wengi ambao wanafanya majukumu wakati yeye yupo kwenye shughuli zingine za taasisi.
Ten amesisitiza kuwa masuala ya benchi la ufundi kupangiwa kikosi yameshapitwa na wakati, kwasababu benchi lina uwanja wake mpana wa kufanya maamuzi kwenye kikosi ili timu ifanye vizuri hivyo kila mtu afanye majukumu yanayomuhusu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: