Mwanamuziki anayefanya poa na ngoma ya 'Mdundo' Msami baby amesema haoni tatizo lolote la yeye kumsifia mke wa Dogo Janja (Irene Uwoya) kwa madai wana historia ndefu ya maisha yao ya nyuma kabla ya kuolewa hivyo haitokuwa rahisi kuacha kumsifia.

Msami ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV baada ya wawili hao kuzua ngumzo mitandaoni kwa kile kilichoonekana kuwa bado wanatamania kimapenzi japokuwa mmoja wapo amekuwa mke wa mtu kwa sasa.

"Ni kweli Uwoya anapenda ninachokifanya ndio maana ameni-post ni kweli kwani kuna kitu gani cha uongo hapo wakati amezungumza ukweli. Kama kucheza ninacheza kwa hiyo anahaki ya kusema anachotaka. Na mimi kuandika mtu fulani ni mzuri sio dhambi kwasababu kwangu mimi binafsi naona kama upendo wa kumkubali mtu kama yeye alivyoona kuwa mimi ninasifa ya kuwa mchezaji bora", amesema Msami

Pamoja na hayo, Msami ameendelea kwa kusema "mimi namjua Uwoya tokea zamani, kwa hiyo tuna maisha yetu na historia, tunaongea na kutaniana mambo mengi,'so' haviwezi vitu kama hivyo kuanza kupotea tu".
Share To:

msumbanews

Post A Comment: