Msafara wa Simba SC kuelekea Uwanjani Port Said, umezuiliwa na viongozi wa soka nchini humo.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni saa moja tu limesalia kuelea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Al Masry dhidi ya Simba.
Simba wamelazimishwa kupanda basi tofauti na lile walilokuwa wamepangiwa awali, hivyo kusababisha kuleta mzozo.
Aidha, uongozi wa Simba umeshtukia mchezo mchafu wa Waarabu, pengine kunawezekana kukawa kumepuliziwa dawa kwenye basi ambalo wanalazimishwa wapande.
Kitendo hicho kimewafanya Simba kugomea kupanda basi walilolazimishwa wabadilishiwe huku wakiweka msisitizo wa kupanda ambalo lilikuwa kwenye ratiba.
Mechi hiyo itaanza saa 2:30 usiku wa leo.
Post A Comment: