Viongozi watatu waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walioripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam leo, ambao ni ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu na Dk Mashinji, wameachiwa kwa dhamana huku Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Serengeti, John Heche wakibaki polisi kwa maelezo kuwa wamekuwa wakikwepa taratibu za dhamana.
Imeelezwa kuwa, Heche na Mnyika hawakuripoti polisi Machi 16, 2018 ambapo Chadema wamesema sababu ya wabunge hao kutoripoti ni kutokana na kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge mjini Dodoma.
Aidha, viongozi wengine wa chama hicho waliotakiwa kuripoti polisi leo Machi 22, ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye yupo nje ya nchi kwa matibabu na Ester Matiko ambaye yuko Dodoma kwa shughuli za kibunge
Post A Comment: