Serikali ya Korea leo imeikabidhi  msaada wa dawa  zenye thamani ya Shilingi Milioni Mia Moja kwa Serikali ya Tanzania ikiwa ni ishara ya mahusiano mazuri kati ya nchi hizo mbili.
Msaada huo umekabidhiwa kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Profesa Joyce Ndalichako jijini Dar es Salaam ili zitumike katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS) Kampasi ya Mloganzila.
Mara baada ya kupokea msaada huo Waziri Ndalichako ameishukuru Serikali ya Korea kwa msaada huo na kuwataka wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho kutumia vema miundombinu ya Chuo kwa  kujifunzia na kufundishia ili kujijenga kitaaluma kwalengo la  kumaliza tatizo la uhaba wa Madaktari na Wataalam wa Afya hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano ya dawa hizo Kiongozi wa Ujumbe wa Korea  wa Kamati ya Afya na Huduma za Jamii ya Bunge la nchi hiyo, Jun Hey Sook amesema msaada huo wa dawa ni ushirikiano katika kuboresha sekta ya Afya.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano serikalini,
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

7/3/2018


Share To:

msumbanews

Post A Comment: