Mchekeshaji kutoka kundi la Timamu, Ebitoke ameibuka na kudai kuwa mahusiano yake na muimbaji wa Bongo Flava, Ben Pol yapo pale pale.
Akizungumza na Bongo5 mchekeshaji huyo amesema wale waliokuwa wakidhani kuwa mahusiano yao ni kiki wanapaswa kuelewa kuwa penzi lao bado linachanua.
“Ben Pol watu walijua mimi na yeye hatuna mahusiano na watu wameshakariri kuwa ni kiki tuacha waendelee na mtazamo ambao wanauona lakini mimi na Ben Pol tunaendeleza mahusiano yetu kimya kimya,” amesema Ebitoke.
Ameongeza kuwa Ben Pol bado anamsaidia mambo mbalimbali katika sanaa yake kama alivyomuhaidi wakati wanaanza mahusiano yao.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: