Baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuonya wanaotaka kufanya maandamano, Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema amesema kuwa kauli aliyoitoa sio ya bahati mbaya.
Lema amemuhoji Waziri Nchemba akisema kuwa “unasema kuna watu wanapanga mauaji ili kuichafua taswira ya Nchi huku akisema kuwa maelekezo uliyo nayo ni kumbambikia Mh Mbowe kesi ya Mauaji”.
“Mwigulu,kauli yako Singida sio ya bahati mbaya.Unasema kuna watu wanapanga mauaji ili kuichafua taswira ya Nchi, maelekezo uliyo nayo ni kumbambikia Mh Mbowe kesi ya Mauaji pamoja na Viongozi wengine, huu Mpango wenu mnaonekana bado mnao.Hivi Dr Kipilimba bado anahubiri Injili”? amehoji Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Waziri Nchemba jana alimuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwakamata watu wote wanaopanga mipango ya kuandamana.
Post A Comment: