Polisi katika wilaya ya Mpigi wamemkamata mzee moja mwenye umri wa miaka 69 anayejulikana kwa jina la Vicent Ssenonga, ambaye ni mganga wa kienyeji kwa kumpa ujauzito binti yake wa kumzaa mwenyewe.
Kwa mujibu wa polisi wa kituo cha Buwama ambako mzee huyo anazuiliwa, wamesema walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa mzee huyo anamnyanyasa binti yake huyo ambaye amemgeuza mke wake, aliyeanza kufanya naye ngono tangu akiwa na miaka 13 mpaka sasa ana miaka 20, huku wakiwa wamezaa watoto watatu.
“Kumuoa na kumtesa mtoto wake mwenyewe, kiasi kwamba hampi chakula na huduma za afya, hatukuweza kuvumilia na kwenda kumchukua huyu mzee. Tumeambiwa kuwa amemtumia huyu binti kwa miaka 7 sasa tangu akiwa na miaka 13, na tunachunguza taarifa kuwa amemuambukiza HIV”, amesema Bwana Jospeh Kakama ambaye ni polis wa zamu wa kituoni hapo.
Naye mwenyekiti wa kijiji Bwana Robert Ssemuju amesema mganga huyo alikuwa akiishi na binti yake huyo pekee, baada ya kuwapa talaka wake zake sita, na watoto wake kutawanyika kutafuta maisha huko Kampala na sehemu zingine.
“Ssenonga amekuwa akimtishia huyu binti asiseme chochote kwa watu, lakini kutokana na afya yake ambayo inadhoofu kila siku, ameamua kutuambia na kuamua kuweza kumsaidia yeye na hawa watoto watatu”, amesema mzee huyo ambaye ni mwenyekiti wa kijiji.
Post A Comment: