Klabu ya Barcelona imetinga robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa kuichapa Chelsea goli 3-0 .
Magoli ya Barcelona yamefungwa na Lionel Messi ×2 na moja likifungwa na Dembele.
Kwa upande mwingine Kocha wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amesema kuwa klabu yake haikustahili kupata matokeo hayo kutokana na uwezo waliyouonesha uwanjani.
“Hatukuwa na bahati goli tuliloruhusu dakika ya pili limegeuza matokeo, ingawaje ukiangalia mechi zote mbili tumepata nafasi za wazi lakini nyingi hatujazitumia vizuri mipira imeishia kugonga milingoti,”amesema Conte na kulalamikia mwamuzi.
“Nadhani tulistahili kupata penati na ilikiwa ya wazi baada ya Marcos Alonso kukwatuliwa na Pique japo sio sababu ila ingewaongezea Barcelona presha,”amesema Conte kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari baada ya mchezo wa Jana kumalizika.
Barcelona na Bayern Munich jana usiku zimeungana na timu nyingine 6 kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambapo droo yake inapangwa kesho Ijumaa Machi 26, 2018.
Post A Comment: