Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Laikipa Mshariki nchini Kenya Mathew Lempurkel, amekamatwa tena na polisi nchini humo, baada ya kuachiwa siku ya tarehe 12 machi, kwa tuhuma za kupanga mauaji.
Kwa mujibu wa Polisi wa Laikipa Kaunti Kamanda Simon Kipkeu, bwana Lempurkel ambaye alikuwa mbunge kupitia chama cha ODM, atafikishwa mahakamani baada ya wapelelezi kukamilisha taarifa zao.
Lampurkel alikamatwa baada ya kutishia kukichoma moto kituo cha polisi cha Rumuruti, kwa lengo la kumtoa mtuhumiwa ambaye alikuwa mahabusu mwezi Julai, 2016.
Mahakama iliamua kuwa Lampurkel ana kesi ya kujibu juu ya vurugu alizofanya, na kisha kukamatwa tena kwa tuhuma za kupanga njama hizo za mauaji.
Post A Comment: