Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa masharti ya dhamana kwa viongozi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili na bondi ya Tsh. Milioni 20.
 
Pia wadhamini hao wawe na barua za utambulisho ambapo baada ya kutimizwa masharti hayo Mbowe na wenzake wawe wanaripoti Central Police mara moja kwa wiki, hata hivyo viongozi hao wameshindwa kutoka baada ya kutofika mahamani kufuatia gari lilokuwa likiwapeleka mahakamani kuharibika.
Wakili wa serikali, Faraja Nchimbi ameieleza Mahakama ya Kisutu kuwa watakata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama hiyo kutoa masharti ya dhamana kwa Mbowe na wenzake.
Viongozi wa Chadema waliokuwa wakishikiliwa ni pamoja na Freeman Mbowe, John Mnyika , Ester Matiko, Salum Mwalimu, Peter Msigwa na Dkt. Vicent Mashinji.
Katika hatua nyingine Wabunge na Madiwani wa Chadema wameandamana kwenda ofisi za Umoja wa Ulaya (EU), viongozi hao wamekwenda katika ofisi hizo kulalamikia kile wanachofanyiwa viongozi wao sita walio na kesi mahakamani.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema, “Tuko EU (Umoja wa Ulaya). Tupo wabunge wote tumeandamana kuja hapa kuleta kilio chetu.”
Share To:

msumbanews

Post A Comment: