Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars Salum Mayanga, leo ametaja majina ya wachezaji 23 watakaoingia kambini kwaajili ya michezo miwili ya kirafiki mwezi huu.
Katika orodha hiyo aliyoitaja asubuhi hii kwenye makao makuu ya shirikisho la soka nchini TFF Karume Ilala, Mayanga amewajumuisha kikosini nyota wanne wa kimataifa akiwemo nahodha Mbwana Samatta.
Wengine waliotajwa ni Thomas Ulimwengu anayechezea klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden, Mlinzi wa Baroka FC ya Afrika Kusini Abdi Banda pamoja na Faridi Mussa anayechezea Club Deportivo Tenerife ya Hispania.
Katika majina hayo 23 Simba imeongoza kwa kuchangia wachezaji wengi zaidi ambao ni 6 huku Yanga ikitoa wachezaji 5 huku nahodha wa Singida United Mudathir Yahya naye akijumuishwa kikosini.
Taifa Stars inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki ikianzia ugenini nchini Algeria Machi 22 dhidi ya wenyeji, The Greens kabla ya kurejea nyumbani, Dar es Salaam kuwakaribisha DR Congo Machi 27 Uwanja wa Taifa.
Post A Comment: