Afisa Habari wa Klabu ya Simba Haji Manara amerusha dongo hewani kwa kusema kuna kikundi kichache cha watu walioijua wekundu wa Msimbazi na Yanga katika mitandao ya kijamii na ndio maana wanaleta chuki za kijinga baina yao bila ya kujua wametoka wapi.

Manara ametoa kauli hiyo asubuhi ya leo kupitia ukurasa wake wa kijamii ikiwa imeambatana na 'video' iliyokuwa inamuonesha mchezaji Haruna Ninyonzima (Simba), Thabani Kamusoko (Yanga) pamoja na Hamisi Tambwe (Yanga) wakiwa wanafanya mazoezi ya viungo katika 'gym' moja bila ya kujali tofauti ya itikadi zao za michezo.

"Very nice', hawa ni 'proffesional player' hasa wanacheza timu shindani kwenye soka nchini, wanatoka mataifa tofauti lakini wapo 'Gym' pamoja hii ndio soka. 'Always' nawaambia Simba na Yanga ni washindani wa dakika 90 za uwanjani na watani wa jadi tu", amesema Manara.

Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "chuki za kijinga zinaletwa na washamba waliozijua hizi timu katika mitandao ya kijamii kama 'facebook', 'WhatsApp na 'Instagram'. Niwatakie heri magwiji wetu".

Kwa upande mwingine, Simba kwa sasa inaongoza katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa na alama 46 sawa na watani wao wa Jadi Yanga zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa pamoja na idadi ya michezo Yanga ikiwa mbele kwa mchezo mmoja
Share To:

msumbanews

Post A Comment: