Mtayarishaji mkongwe wa muziki wa BongoFleva, Man Water amefunguka na kuwahakikishia mashabiki wa Alikiba kuwa kuna ngoma mpya imeshafanyika mpaka 'video' na muda wowote kutoka sasa inaweza kuachiwa ili kuvunja ukimya uliokuwepo kwa kipindi kirefu.
Man Water amebainisha hayo wakati alipokuwa anapiga stori na 'BIG CHAWA' kutoka katika kipindi cha Planet Bongo 'PB' ya East Africa Radio baada ya kuwepo na malalamiko mengi yanatoka kwa mashabiki wake waliokuwa wanadai wanataka kumsikia mfalme wao aking'uruma katika muziki. 
"Kuna ngoma ambayo tumefanya na imeshafanyiwa video tayari kwa jinsi nilivyosikia, kwasababu Alikiba yupo South Afrika 'SA'. Pengine wimbo huo unaweza ukawa ndio unaofuata kwa sasa baada ya 'Seduce me", amesema Man Water.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: