Klabu ya Manchester United usiku wa kuamkia leo umewakumbusha mashabiki wake katika kipindi cha miaka ya nyuma ambapo ulikuwa huwezi khakikisha umwafunga mpaka usikie firimbi ya mwisho ya muamuzi wa mchezo.

Katika mchezo huo wa jana waliocheza na Crystaal Palace katika uwanja wa ugenini wa Selhurst Park, United walifanikiwa kutoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Mabao hayo ya Man United yalifungwa na Chris Smalling dakika ya 55, Lukaku dakika ya 76, na Nemanja Matic kwenye dakika ya 90.
Crystal Palace walianza kuongoza kwa kufunga mabao yao kupitia kwa Andros Townsend dakika ya 11 na Patrick van Aanholt dakika ya 48.
Kutokana na matokeao hayo United wanaendelea kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu Uingereza wakiwa na alama 62, wakati huo huo Manchester City ndio anaongoza ligi hiyo akiwa na alama 78 wakati Palace anashika nafasi ya 18 akiwa na alama 27.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: