MANCHESTER United inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Liverpool, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Old Trafford, mchezo huo ni mkubwa na unasubiriwa kwa hamu.
Kuelekea mtanange huo, gumzo kubwa ni juu ya uwezo wa kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ambapo mashabiki wa United wameanza kupata hofu kuhusu mchezaji ambaye atamzuia.
Kawaida Salah amekuwa akipangwa kushambulia akitokea kulia, kwa aina ya ulinzi wa United beki wa kushoto ambaye atatakiwa kukutana naye ni Ashley Young au Luke Shaw, sasa hapo ndipo patamu, imeibuka hoja juu ya nani mwenye uwezo kati yao anayeweza kumficha Salah.
Mchezo uliopita timu hizo zilipokutanaa ulimalizika kwa suluhu, huku Marteo Darmian akipangwa kucheza beki wa kushoto, kwa sasa beki huyo siyo chaguo la kwanza la Kocha Jose Mourinho.
Kutokana na ubora wa Salah kufunga, mashabiki wa United kutoka mataifa mbalimbali wamepaza sauti wakitoa maoni kuwa ni bora akaanza Shaw kwa kuwa ni beki halisi wa kushoto na hatatakiwa kupanda mara kwa mara, huku wakidai Young ambaye ndiye anayetumika mara nyingi siyo beki halisi mchezo uliopita United ilicheza mbinu y a kuzuia zaidi kitendo ambacho kilimkera Kocha wa Liverpoo, Jurgen Klopp. Kwa sasa United haitarajiwi kuendeleza staili hiyo kwa kuwa inahitaji ushindi na ipo nyumbani.
Liverpool ina kasi kubwa ya kufunga mabao lakini imekuwa ikiruhusu kufungwa mabao mengi pia tofauti na United ambayo imekuwa ngumu kufungika hasa inapokuwa nyumbami,Young ni winga lakini amekuwa akitumika kama mlinzi wa kushoto.
Mbali na Salah mastaa wengine wa Liverpool ambao watatakiwa kuchungwa ni Sadio Mane na Roberto Firmino ambao wamekuwa na kasi kubwa ya kufunga hivi karibuni.
Post A Comment: