MAMA
mwenye mtoto mwenye nguvu za ajabu anayeishi Mtaa wa Kwa Mbela uliopo
Mburahati Mianzini Salama Omar amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Paul Makonda kumsaidia katika matibabu ya mwanaye.
Mbali
ya kumuomba Makonda kumsaidia matiabu ya mtoto wake Mzamiry Said(7),
pia ametumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo mumewe aliyefunga naye
ndoa mwaka 2009 alivyomtekeleza yeye na mtoto.
Akizungumza
na Michuzi blog leo jijini Dar es Salaam Salama amesema anaishi maisha
yenye changamoto nyingi anakabiliana nazo katika malezi ya mtoto wake
ambaye ameeleza amekwenda kwenye hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali
ya Taifa Muhimbili na CCBRT.
Amefafanua
na kote huko alikokwenda madaktari wamechukua vipimo vyote vikiwemo vya
kuangalia iwapo ana tatizo la akili au ulemavu lakini wamemthibitisha
matatizo hayo ila anakumbuka mmoja wa madaktari wa Muhimbili
anayeshughulikia watu wenye magonjwa ya akili anakumbuka alimwambia
mwanaye hata pona , hivyo ataendelea kuwa hivyo katika maisha yake yote.
"Ni
kweli mwanagu sasa ana maiaka saba na tatizo bado lipo.Ana nguvu nyingi
na anapocheza na wenzake unakuwa makini kufuatilia maana anaweza
kufanya chochote ambacho si kizuri. Napata shida kwenye malezi ya
mwanangu tangu alipozalizwa.
Nimejitahidi
katika matibabu lakini hali iko vile vile.Muda wote inabidi niwe
namchunga asiende mbali kwani unaweza kumuacha akaenda kucheza na watoto
wengine mtaani lakini kutokana na nguvu alizonazo anaweza hata
kujeruhi.
"Kuna
wakati anaweza kukaa lakini ghafla ukamuona anaanza kukimbia ,hivyo ili
nimshike natumia nguvu nyingi sana maana anaweza kunishika mkono na
nikashindwa kuutoa.Kote mtaani hadi Serikali za mitaa wanamjua na
matatizo yanayomkabili.Kwa kweli nahangaika sana na malezi ya mtoto,
sina wa kunisaidia na kwa kuwa muda wote nipo nakosa hata nafasi ya
kwenda kutafuta fedha kwa ajili ya
kula.
"Moyo
wangu unanisukuma na kuamini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam atanisaidia
na nipo tayari kupokea msaada wa aina yoyote atakaoamua kunisaidia iwe
matibabu au chakula .Makonda ni kiongozi anayeguswa na shida za watu na
naamini hata mimi akisikia kama taarifa hizi ataziona naomba anisaidie
na Mungu atamlipa kwa kile ambacho atakifanya kwa ajili ya
wanangu,"amesema Salama.
"Kuhusu
hili la mume wangu kunitelekeza na mtoto, natamani kwenda kwa Makonda
pia kwa ajili ya kupata maada wa kisheria kwani tangazo lake la kuagiza
wanawake waliotelekezwa na waume zao waende kwake nimelisikia lakini
sasa sina mtu wa kumuachia mtoto.
"Mkuu
wangu wa mkoa naomba nisaidie ili itoke kwenye changamoto za
kimaisha.Mtoto aahitaji eneo lenye utulivu kwani akiona watu ndio kama
vile anachanganyikiwa na nguvu za ajabu zinamjia,"amesema.
Kuhusu
aina ya maisha ambayo anaishi kwa sasa anasema bado anaendelea kutafuta
matibabu kwa ajili ya mwanaye kwani hajakata tamaa na anaamini ipo siku
Mungu atamuondolea maradhi na kusisitiza anaamini msaada wa Makonda
iwapo atamsikia anaweza kumsaidia.
Post A Comment: