Kituo cha Redio Times FM cha jijini Dar es salaam leo Machi 22, 2018 kimethibitisha kupokea barua kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo imekitaka kituo hicho kuwasilisha kipindi cha The Playlist kilichorushwa Machi 19 mwaka huu.
Akielezea jambo hilo Mkurugenzi wa Times FM, Amani Misana amesema kuwa leo Machi 22, 2018 wamepokea barua hiyo na tayari wameshawasilisha kipindi hicho TCRA .
Tumepokea barua na tumefanya yale tuliyoagizwa ikiwamo kuwasilisha kipindi chote,” amesema Misana kwenye mahojiano na MCL Digital.
Jumatatu ya Machi 19, 2018 msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz alizua mjadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya kunukuliwa kwenye mahojiano yake na kituo hicho cha Redio akimlalamikia Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Juliana Shonza kuwa anafanya uonevu kwa kufungia nyimbo za wasanii.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: