Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR), imesema Mahakama za ndani Tanzania katika kesi ya kubaka na kulawiti iliyokuwa inamkabili mwanamuziki Babu Seya na mwanawe Papii Kocha, zilitenda haki kwa kiwango kikubwa na kwa upande mwingine zilikiuka.
“Kutokana na kukiukwa kwa baadhi ya haki za Seya (Babu Seya) na Johnson (Papii Kocha), mahakama imewaruhusu kuwasilisha hoja na kuainisha ni namna wanaweza kuomba fidia kulingana na haki zao ziliokiukwa ndani ya siku 30,”- Jaji Gerald Niyungeko, Mahakama ya Haki za Binadamu,
“Baadhi ya haki zilizotendwa ni pamoja na kuwaachia watuhumiwa watatu kwenye kesi hiyo pamoja na kubakiza mashitaka manne kati ya 21 yaliyokuwa yakiwakabili,” Jaji Gerald Niyungeko, Mahakam ya Haki za Binadamu
“Kwa upande mwingine haki zao zilikiukwa, kwa mfano wakiwa Mahakama ya Kisutu walikaaa mahabusu kwa siku nne bila kufahamishwa makosa yao lakini pia hawakuwa na wakili wa kuwatetea,”- Jaji Gerald Niyungeko, Mahakama ya Haki za Binadamu
“Aidha, waleta maombi pia waliomba kupimwa mkojo na damu ili kuthibitishwa kama waliwaingilia wale watoto ambao upande wa jamhuri ulidai waliambukizwa magonjwa ya zinaa lakini walikataliwa,”- Jaji Gerald Niyungeko
Kwa upande mwingine, Nguza aliomba kupimwa kama ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa au lakini pia alikataliwa,”- Jaji Gerald Niyungeko.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: