Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo akitoa maelekezo kwa
wasanii wa Filamu wa Mkoa wa Arusha wakati wa mafunzo ya kuwajengea
uwezo wasanii wa filamu wa mkoa huo yaliyofanyika jijini Arusha.
Zaidi ya wasanii mia moja wamepatiwa mafunzo hayo.
Afisa
Utamaduni wa Mkoa wa Arusha, Irene Ngao (kushoto) akizungumza na
Wasanii wa Filamu wa Mkoa wa Arusha (hawapo pichani) wakati wa mafunzo
ya kuwajengea uwezo wasanii wa filamu yaliyofanyika jijini Arusha.
Zaidi ya wasanii mia moja wamepatiwa mafunzo hayo.
Wasanii
wa Filamu wa Mkoa wa Arusha wakifuatilia mafunzo ya uandaaji wa filamu
yaliyofanyika leo jijini Arusha, mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Bodi ya
Filamu Tanzania yamehusisha zaidi ya wasanii mia moja.
Kaimu
Afisa Elimu Wilaya ya Arusha Mjini, Antony Mushi akifunga mafunzo ya
kuwajengea uwezo wasanii wa Filamu wa Mkoa wa Arusha yaliyofanyika
jijini Arusha. Mafunzo hayo yameratibiwa na Bodi ya Filamu Tanzania
ambapo zaidi ya wasanii mia moja wamepatiwa mafunzo.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo (wa kwanza kushoto)
akicheza ngoma na wasanii wa kikundi cha ngoma cha Mtikisiko Sanaa Group
cha jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo
wasanii wa filamu mkoani humo mapema hii. Zaidi ya wasanii mia moja
wamepatiwa mafunzo hayo. Picha Zote Na Octavian Kimario WHUSM
Post A Comment: