Maelfu ya vijana mbeya wamemsindikiza kwenye makazi ya milele kijana Allen Mapunda (20) aliyekuwa mfanyabiashara wa machungwa mkoani Mbeya anayedaiwa kufariki muda mfupi baada ya kuachiwa na polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga amesema Jeshi hilo halihusiki kwa namna yoyote na kifo cha Allen ambaye anadaiwa alitoka rumande Machi 25, saa 4 asubuhi na ilipofika saa 12 alifariki dunia.
Awali, Mkuu wa Mkoa Mbeya, Amos Makalaalimuagiza RPC Mohamed Mpinga kuunda kikosi kazi kitakachochunguza tukio zima lilipolekea kifo cha Allen Mapunda. Amesema kikosi hiko kijumuishe wanafamilia na jamii ambayo inamfahamu Allen kisha kumkabidhi ripoti ili hatua zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.
Kijana Allen Mapunda ambaye alikuwa mkazi wa Kata ya Iyela, anadaiwa alifariki Machi 25, 2018 saa chache baada ya kuachiwa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi mkoani Mbeya alipokuwa amekamatwa na jeshi hilo.
Post A Comment: