Wazazi wanapaswa kuwapa nguvu, moyo na kupata haki ya elimu kwani wao pia wanauwezo wa kufanya kazi mbalimbali katika jamii  hivyo katika matembezi hayo yatasaidia kuelimisha jamii kuhusu watoto wenye Usonji(Autism) kuonekana wanaweza na wana haki ya kupata elimu kama watoto wengine.





Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi  wa shule za Almuntazir Mohammad Ladack amesema lengo  la maadhimisho hayo ni kuelimisha jamii kuhusu watoto wenye Usonji (autism) na kuondoa dhana ya kuwaona watoto hao kama hawawezi hivyo wametakiwa kuwapa nafasi ya kufanya na kuona umuhimu wao katika jamii.


"Wazazi tunapaswa kuwapa nafasi watoto hawa na kuona kuwa wanaweza kufanya na wanahaki ya kupata elimu hivyo wazazi wawape nafasi ya elimu kwani wanaweza kufanya mambo mbalimbali hivyo tuwalinde na tuwapende pia" Amesema Mkurugenzi Ladack.




wa upande wake mwalimu wa watoto maalumu Eva Wigira amesema matembezi hayo yana lengo la kuelimisha jamii kuweza kufahamu watoto kama hawa wapo katika jamii na hivyo wana haki ya kupata elimu na wanauwezo mzuri wa kuweza kujifunza na kufanya mambo mbalimbali kwa manufaa yao ya badae.


"Watoto wenye usonji wapo katika jamii zetu hivyo matembezi haya yataelimisha jamii kuhusu watoto hawa kupata elimu pamoja na kuona wanaweza kufanya vizuri katika masomo na mambo mbalimbali baada ya kupata mafunzo ya namna ya kufanya kama tunavyofundisha hapa shuleni kwetu" Amesema Eva Wigira.

Vilevile ikiwa ni siku ya maji wanafunzi wa shule ya Almuntazir Islamic school ya wasichana wamefika kuwapatia maji watoto wenye usonji (Autism) ikiwa ni ishara ya kuwatia moyo na kuwafanya wajione ni sawa na wengine hawapaswi kutengwa wala kuonekana hawezi.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Makamu mkuu wa shule ya wasichana  Joan Soka amesema watoto hao wametembea lengo likiwa ni kuelimisha na kuwawezesha kufahamu maana ya usonji  pamoja na kuwatia moyo watoto wenye Autism na kuwafanya kuona wanakubalika katika jamii na ni muhimu kama wengine.

Amesema wazazi wanapaswa kuona umuhimu wa watoto hawa wanapaswa kupewa elimu na kuona ni changamoto ya kila mzazi kuwapenda na kuwalinda watoto wenye usonji (Autism) hivyo amewataka wazazi na wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika matembezi hayo.

Matembezi hayo yatafanyika siku ya Jumapili tarehe 25, March mwaka huu ,ambapo yataanza muda wa saa moja na nusu asubuhi katika barabara ya Obama
Share To:

msumbanews

Post A Comment: