Msanii wa BongoFleva ambaye anatamba na kibao chake cha 'amezoea', Lulu Diva amesema hapendi kuona baadhi ya watu wanashindanisha kazi zake za muziki na Shilole kwa madai kitendo hicho kinaweza kuwagombanisha jambo ambalo kwake halitaki liwe hivyo.

Lulu Diva ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya baadhi ya watu kuanza kufananisha na kushindanisha kazi za wasanii hao wawili ili mwisho wa siku apatikane aliyekuwa juu zaidi ya mwenzake.

"Hakuna hata siku moja mtu anakuja na kupotezwa, kila mtu anaimba muziki wake na mimi Shilole namuheshimu kama dada yangu na anafanya muziki wa aina yake. Ukiangalia anachokifanya Shilole na Mimi ni vitu viwili tofauti", amesema Lulu Diva.

Pamoja na hayo, Lulu Diva ameendelea kwa kusema "ni watu tu wanajaribu ku-creaty vitu ili wajaribu kutuchonganishi baina yetu ninaomba hivyo vitu visiendelee kuwepo maana ninamuheshimu sana Shilole katika muziki amenitangulia na anajua mengi zaidi yangu. Mimi sifanyi muziki wa mwanamuziki yeyote kila mtu ana muziki wake".
Share To:

msumbanews

Post A Comment: