Serikali kupitia Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari – Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas imesema baada ya kuanza kuleta ndege nchini kuna watu roho ziliwauma wakati ni Tanzania ni nchi ambayo ilikuwa inalalamika hakuna shirika la ndege na halina ndege zake.
Dkt. Abbas ameyasema hayo leo, wakati akijibu swali la mwandishi wa habari aliyehoji kushikiliwa kwa ndege moja ya Tanzania nchini Canada ambapo ameeleza kuwa kuna wafitini na wazandiki wakioona nchi inaendelea wanaumia na inshallah watashindwa .
“Ni kweli kwamba ndege yetu watu walichomeka huko umbea na unafki watu wakaenda wakajenga hoja wakafikiri tutalipa kwa kubabaika au kutetemeka hapana sisi tuko makini, kwahiyo mzee ndege zetu zote mwezi wa saba zitakuwa Tanzania na usiseme ya Canada kwamba ni moja ndege zetu zote hii zote zinatengenezwa na kampuni ya Bomberdier ya Canada tuendelee kupeana updates kwamba ikifika July zimefika ngapi ambayo haijafika tutasema ile ndege tulishasema wafitini wanaodhani Tanzania wao inauma sasa waendelee kuumia,“amesema Dkt. Abbas.
“Ndege zinakuja na zitafika nchi hii na baadhi yenu mtazipanda mtakao kwenda lakini hilo liko wazi kabisa kuna watu waliona nchi hii sasa imeanza kuwa imara, katika nchi ambayo tulikuwa tunalalamika hatuna shirika la ndege halina ndege zake tunaanza kuleta watu roho ikawauma tulishasema hilo liko wazi kabisa kuna wafitini na wazandiki wanaoona tuna move kutoka sehemu moja kwenda nyingine sasa inshallah watashindwa.“
Post A Comment: