Klabu ya Simba ambayo iliondoka jana usiku nchini Tanzania kuelekea Misri kwa ajili ya mechi ya marudiano na klabu ya Al-Masry kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho, Klabu hiyo imewasili salama nchini humo.
Simba SC wametua mjini Port Said nchini Misri wakipitia Addis Ababa nchini Ethiopia, ambapo wakiwa huko wamekutana na balozi wa Tanzania nchini humo, Meja General Issa Suleiman Nassor na kupewa baraka zote.
Simba na Al-Masry walitoka sare ya goli 2-2 kwenye mchezo wa kwanza ambao ulipigwa hapa Tanzania na watahitaji ushindi kwa namna yoyote au sare ya kuanzia goli 3 ili waweze kusonga mbele
Post A Comment: