Kesi ya kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe , Halima Mdee imeshindwa kuendelea baada ya mshtakiwa kuwa magonjwa na kuahirisha kesi hiyo hadi Mei 3, 2018.

Leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wadhamini wa Mdee, Fares Robison ambaye ni Diwani wa Mbezi Juu na Martha Mtiko (diwani wa viti maalumu), wameieleza mahakama hiyo kuwa Mdee yupo Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.

Mbele ya ya Hakimu Thomas Simba, Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amedai kuwa shauri hilo leo limefika kwa ajili ya kuendelea na ushahidi ambapo Mdee anakabiliwa na shtaka moja la kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais , John Magufuli kwa kusema, “anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afungwe breki”.

Baada ya maelezo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 3, 2018 itakapoendelea na ushahidi.

Mdee anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 4, 2017 katika Makao Makuu ya CHADEMA yaliyopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: