Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Nape Nnauye amefunguka na kudai kutohusika na kupanga mambo mbali mbali yanayoendelea nchini baada ya kutuhumiwa kufanya hilo na mmoja wa raia.

Nape Nnauye amefunguka hayo wakati akijibu moja ya hoja ya mtu aliyemtuhumu yeye kama Mbunge wa CCM na kusema kiongozi huyo anajua na kuona haki za raia zikivurugwa

"Naamini unaitwa Kusiluka,nimesoma lawama zako kwangu,una haki ya kulaumu ili upumue, lakini kuna kikao nimeshiriki kupanga hayo unayonituhumu?! Nadhani kuwa mkweli kwa nafsi yako tuhuma hizo ni nzito si sawa kuzisema bila kuwa na hakika, sihusiki na hayo usemayo na nayalaani pia" Alidai Nape Nnauye

Nape Nnauye aliwataka Watanzania kwa pamoja kuwasha mishumaa ya matumaini na hapo ndipo mtu huyo alipoibuka mwananchi huyo na kusema kuwa kiongozi huyo yeye anatambua na kujua kinachoendelea nchini sasa, jambo ambalo Nape Nnauye amelikana na kusema hata yeye analaani kwa vitendo vinavyoendelea nchini
Share To:

msumbanews

Post A Comment: