Na Ferdinand Shayo, Arusha.
Wimbi la Viongozi kutoka CHADEMA na kuhamia CCM linaendelea jijini Arusha ambapo licha ya madiwani wanaojiuzulu kila kukicha,Leo Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Arusha Gabriel Kivuyo amekihama chama hicho na kuamia CCM.
Kigogo huyo amepokelewa katika ofisi za CCM wilaya na Katibu wa CCM wilaya Musa Matotoka Aliyongozana na makada wengine wa CCM wakishuhudia zoezi la kukabidhiwa kadi la Kivuyo.
Aidha ametaja sababu za kujiuzulu ni pamoja na kutokupata ushirikiano kwa baadhi ya viongozi akiwemo mbunge hivyo haoni sababu ya kuendelea kuwepo katika chama hicho.
Pia ameshutumu vikali kitendo cha kutolewa kwenye kikao cha Mameya ambapo walimtuhumu kuwa anawarekodi.

Post A Comment: