Msanii wa muziki BongoFleva Juma Jux ambaye yuko kwenye mahusiano ya kimapenzi na Vanessa Mdee, amekanusha taarifa za mpenzi wake huyo kuwa mjamzito na kudai kwa sasa hawajajipanga kufanya hivyo ila endapo watakuwa tayari kwa hilo watasema.
"Kiukweli Vanessa hana ujauzito ile ni picha tu, labda siku hiyo alikuwa ametoka kula 'ameshiba' na kupigwa picha vibaya ndio ikatokea hivyo. Lakini hakuna kitu kama hicho, hivyo vitu inabidi viende kwa mipango pia lazima mwenzako umshirikishe endapo unataka kufanya hivyo na mkubaliane ili mambo yaweze kwenda sawa", amesema Jux.
Pamoja na hayo, Jux ameendelea kwa kusema "ikifika 'time' watu watajua kwasababu sisi hatuwezi kuficha mambo hata kama sisi hatuto-post lakini inaweza akaja ku-post mtu mwingine kwa kutuona sehemu fulani".
Jux kwa sasa anafanya vizuri kibao chake kipya kilichopewa jina la 'fimbo' aliyoachia siku za hivi karibuni
Post A Comment: