Rais wa nchi ya Marekani, Donald Trump amemteua John Bolton kuwa mshauri mkuu kuhusu masuala ya usalama wa taifa.
John Bolton anachukuwa nafasi hiyo ambayo hapo awali ilikuwa ikishikiliwa na Luteni Jenerali Herbert Raymond McMaster ambaye aliyefutwa kazi.
Bolton, 69, aliwahi kuwa waziri wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa na anakuwa mtu wa tatu kukalia kiti hicho katika kipindi cha takribani miezi 14 ya utawala wa Trump.
Bolton ni mtu muhimu kwa Marekani kwani alisaidia kuibua madai ya kumiliki silaha dhidi ya Saddam Hussein aliyekuwa akituhumiwa kumiliki silaha za maangamizi.
Awali nafasi hiyo ilikuwa ikikaliwa na Michael Flynn ambaye alijiuzulu kufanya kazi hiyo kwa wiki tatu tangu alipoteuliwa na Trump na nafasi yake ilichukuliwa na Luteni Jenerali Herbert.
Post A Comment: