Watazamaji wataingia bure katika mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes na vijana wenzao wa Morocco Leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa Jana mjini Dar es Salaam na Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maandalizi ya mchezo huo utakoanza Saa 10:00 jioni.
Ngorongoro iliyo chini ya kocha Ammy Ninje, itakuwa na mechi mbili za kirafiki na mbali na hii ya Leo, nyingine itafuatia Jumatano ya Machi 21, dhidi ya Msumbiji.
Kwa Ngorongoro mechi hizo ni maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la mataifa ta Afrika (AFCON U20) dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Machi 31 Uwanja wa Taifa na marudiano wiki mbili baadaye mjini Kinshasa.
Ngorongoro Heroes imeingia kambini katika Hoteli ya Ndege Beach iliyopo Mbweni ambapo inajiandaa na michezo hiyo miwili ya kirafiki na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 20.
Ninje anapewa Ngorongoro baada ya kuweka rekodi mbaya kwenye Challenge nchini Kenya mwaka jana, Kili Stars ikiondoka bila kushinda hata mechi moja, ikiambulia sare moja na kufungwa mechi zote. Katika michuano hiyo, pamoja na Ninje kuboronga, aliwakera Watanzania kwa majibu yake.

Post A Comment: