Afisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka na kudai kuna baadhi ya watu wanamuombea dua mbaya ili afariki kwasababu amekuwa ni mtu wa kusifia wachezaji kutoka katika timu yake na kuwaponda kutoka vilabu vingine.
Manara amebainisha hayo jioni ya leo (Machi 28, 2018) kupitia ukurasa wake maalum wa kijamii na kusema hatoweza kuacha kuwasifia wachezaji wake kwa kuwa ni moja ya wajibu wake aliokuwa nao kama msemaji wa timu.
"Kuna watu wachache waliojua soka Instagram wanatamani nife eti kwa kuwa ninasifia sana wachezaji wangu, nawaambia sitaacha kwa kuwa hii ni moja ya wajibu wangu kama vile ninavyowasifia wa timu nyingine wanapofanya vema au kama nyie mlivyowasifu walioshushwa na Mungu", amesema Manara.
Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "kadri mnavyoumia mimi ninazidi kuwachoma,halafu 'guys why' muhangaike na huu ukurasa ?. Hata kama mimi maarufu sio kihivyo si muende kwa msemaji wenu jomoni au kule miyeyusho na Wallah msipokuja ku-like na ku-comment nahama nchi".
Kwa upande mwingine, hicho alichokisema Manara baadhi ya watu wamedai amewalenga moja kwa moja watani zake wa Jadi Yanga kutokana na kuunganisha matukio yanayohusu timu hiyo.
Post A Comment: