Hapo jana siku ya Ijumaa kulienea kipande cha video kinachowaonyesha wachezaji wa klabu ya Yanga, Thaban Kamusoko, Amis Tambwe na Haruna Niyonzima wa Simba SC wakiwa pamoja katika mazoezi ya viungo Gym.
Kufuatia video hiyo msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ameibuka na kusema kuwa licha ya wachezaji hawa kucheza timu mbili pinzani za Simba SC na Yanga SC lakini wapo pamoja na hivyo ndivyo soka linavyo hitaji.
Very nice..hawa ni pro hasa..wanacheza timu shindani kwenye Soka nchini..wanatoka mataifa tofauti..lakini wapo Gym pamoja…hii ndio Soka..always nawaambia Simba na Yanga ni washindani wa dak 90 na watani wa jadi tu..chuki za kijinga zinaletwa na washamba walozijua hz timu FB. WhatsApp na Instagram..niwatakie heri magwiji wetu…. @thabani_scara_13@tambwe17 @niyonzimaharuna
Wachezaji, Thaban Kamusoko na Amis Tambwe wa Yanga SC wapo katika mazoezi mepesi kufuatia kutoka katika majeruhi yaliyokuwa yakiwasumbua kwa muda mrefu wakati kiungo wa Simba SC, Haruna Niyonzima alikuwa akisumbuliwa na kifundo cha mguu kilicho mpelekea hadi kupelekwa nchini India kwa matibabu na hatimaye kurejea nchini.
Post A Comment: