Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Timu ya Simba, Haji Manara amefunguka na kuweka wazi kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ni moja kati ya vitu ambavyo vinaleta chuki na ugombanishi wa serikali na wananchi. 
Haji Manara amesema hayo kupitia moja ya mtandao wake wa jamii na kusema kuwa TANESCO wamekuwa tatizo kubwa kwani wamekuwa wakikata kata sana umeme bila sababu 
"Kama kuna ugombanishi mkubwa unaofanywa kwa watu wa mijini na Serikali yao basi ni huu unaofanywa na TANESCO, mimi ninaishi Magomeni hapa jijini. Ila haijawahi kutokea umeme uwake siku tatu mfululizo bila kukatika Jumatatu iliyopita ulikatika kwa saa 48 mfululizo. umerudi jana, leo mida hii washauchukua..inakera na inasikitisha sana tena sana. Mh RC Paul Makonda. DC Ally Hapi. Waziri mwenye dhamana ya Nishati mnao watendaji katika baadhi ya mashirika ya umma wanafanya kusudi ili wananchi waichukie Serikali yao makini...naomba mtusaidie kwa hilo TANESCO Rais Magufuli na  Dkt.Medard Kalemani" alisema Haji Manara 
Hata hivyo jana Machi 22, 2018 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amempa siku 14 Meneja wa TANESCO mkoa wa Temeke, Mhandisi Alex Adam kuhakikisha anafanya marekebisho ya miundombinu iliyochoka na kusababisha umeme kukatika katika maeneo ya Mbagala na Kigamboni jijini Dar es Salaam
Share To:

msumbanews

Post A Comment: