Rapa Fareed Kubanda ameamua kuchukua jukumu la kuanzisha majadiliano na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuhusu adhabu ambayo wamempa rapa Roma Mkatoliki ikiwa pamoja na kufungiwa kutojihusisha na sanaa kwa muda wa miezi sita.
Fid Q yeye anaamini kuwa muda ambao wamemfungia Roma Mkatoliki ni muda mrefu kwa kuwa ni msanii ambaye ana familia na anaendesha familia yake hiyo kwa kazi ya sanii tu hivyo anaamini kifungo hicho si kizuri kwa msanii huyo.
"Waswahili wanasema "mambo ya kusadifu (kutosheleza haja ) ni ya chunguni ( yale yaletayo faida kama chakula n.k)" Tunaomba mturuhusu tuje tujadili hii sheria ya kifungo upya siku ya Jumatatu BASATA ili kumuokoa baba anayetegemewa na familia kwa kupitia sanaa" alisema Fid Q
Kupitia ombi la Fid Q Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limekubali ombi la msanii huyo kwenda kujadili kwa pamoja juu ya kifungo hicho na masuala mengine ambayo yanahusu sanaa haswa katika muasuala ya muziki na wasaniii.
"Milango iko wazi muda wote. Baraza limesukuma kuundwa kwa umoja wa wasanii ili kujenga mfumo rasmi wa mawasiliano na majadiliano. Bahati mbaya wasanii wengi bado wako nje ya mfumo huu. Limekua likiitisha vikao vya mashauriano, mahudhurio yamekua hafifu. Kupitia umoja uliopo karibuni" ilisema taarifa ya BASATA
Machi 1, 2018 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Daniel Shonza alimfungia msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na masuala ya muziki kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kutofanya marekebisho katika wimbo wao wa Kibamia kama ambavyo walikubaliana awali.
Post A Comment: