MSANII wa filamu nchini Tanzania, Faiza Ally, huenda akawa mmoja wa mastaa ambao wamekasirishwa na kitendo cha mfanyabiashara na aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kupata dili la kutangaza nepi za watoto za Soft Care.
Faiza Ally amesema kuwa ameshangazwa na kampuni hiyo kumtumia Zari kutoka Uganda kwenye matangazo yao wakati kuna Watanzania wengi na wenye majina ambao wangetumika kutangaza bidhaa zao.
Baadhi ya maneno aliyoyasema Faiza kupitia akaunti yake ya Instagram ni kama ifuatavyo:
“I know this is gonna look bad for somepeople but let me be honest , how stupid Tanzanian can be , mastaa wote watanzania , watu wote watanzania hamkuona hata mmoja anae stahili kupata dili zaidi ya zari ? Ina maana uhitaji bongo umeisha mpaka tuweke watu kutoka nje ?? Kwa nini tunawapa kipa umbele wageni tunajizarau sisi ??? Mlishawahi kuona Uganda na kenya wamempa nani dili wakamuacha wa kwao ?? Eti sasa hivi mganda na mkenya wanapongezan na sisi wote tunaonekana hatukufaaa,” ameandika Faiza Ally kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Hata hivyo, Faiza amemshangaa mwanamitindo Noel ambaye yeye ndiye aliyehusika kwa kiasi kikubwa kufanya connections hadi Zari kupata dili hilo.
Katika maneno ya kumlaumu Noel katika akaunti yake ni haya:
“Noel you know all the Tanzania star na uko karibu hukuona anae faa ? I don’t hate zari but I hate kuona vitu wanavyo stahili kupata watanzania kapata mganda this is no good ! Hakuna nchi duniani utaenda ukaona mgeni anapewa kipa umbele zaidi ya mwenyeji , kiasi mpaka ukiwa unasuburi tax mpaka mwenye nchi apate na wewe ndio unafata,” ameeleza Faiza Ally.
Mtazamo wa Faiza umepingwa na baadhi ya Watanzania waliotoa maoni yao kwenye posti yake wakidai kuwa wanawake wengi wa Tanzania wanautumia umaarufu wao vibaya kwa kuuza sura kwenye mitandao badala ya kuwa na wawakilishi wa kuwatafutia madili mbalimbali, kitu ambacho amewazidi Zari.
Post A Comment: