Tanzania imeripotiwa kuwa miongoni mwa nchi zilizopo katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali baada ya baadhi ya wataalamu wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kutoa ripoti ya utafiti wa juu ya ulaji wa nyama ya nguruwe.
Nyama hiyo inayotumika kama kitoweo katika sehemu mbalimbali na yenye majina kadhaa kutoka kwa walaji imedaiwa katika utafiti huo kuwa na madhara ya kiafya kwa walaji.
Hata hivyo utafiti huo wa watalamu wa kisayansi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine wamebaini kuwa watumiaji nyama ya nguruwe wako hatarini kupata magonjwa kadhaa kama vile kifafa kutokana na minyoo ya tegu iliyopo katika nyama hiyo.
Kutokana na utafiti huo watalaam hao wakati wa kuwasilisha tafiti hiyo wameshauri nyama hiyo kupigwa marufuku kutokana na kusababisha magojwa hayo kwa binadamu.
Utafiti huo umetolewa na Dk. Boa Mathias Emanuel ambaye ni mtafiti wa magojwa ya binadamu na wanyama alipozungumza na mwandishi wa BBC.
Aidha, watalaamu hao wamependekeza kuwa kwa wale wote wanaotumia nyama hiyo kuichemsha au kukaanga ili kuviua vijidudu vinavyosababisha ugonjwa huo badala ya kuichoma.
Wamesema kwamba, endapo nyama hiyo itachomwa, joto la kuchoma halitotosha kuangamiza mdudu aliyepo katikati ya minofu ya nyama hiyo kwa sababu upepo unaopita hupunguza joto hilo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: