Mtangazaji maarufu wa kike nchini Tanzania, DJ Fetty ambaye ametangaza habari njema kwa mashabiki wake ambao wali’miss sauti yake redioni kuwa kwa sasa anafanya mazoezi na anatarajia kurudi hewani muda wowote.
DJ Fetty kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii amethibitisha hilo ingawaje hajasema atarudi kutangaza kwenye kituo gani.
Mwaka 2015 Dj Fetty alitangaza kuacha kazi ya utangazaji katika kituo cha Clouds FM ambapo alitoa sababu kuwa anaacha kazi hiyo ili kuendelea na shughuli zake za ujasiriamali.
Hata hivyo, Dj Fetty bado hajatangaza kuwa atarudi kutangaza kituo gani cha Radio/Tv ingawaje mashabiki wengi wanatabiri kuwa huenda akarudi Clouds FM au kujiunga na kituo kipya cha Wasafi FM kinachomilikiwa na msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.
Mwaka 2016 Dj Fetty alinukuliwa akimwambia mtangazaji wa kipindi cha Jahazi, Captain G Habash kuwa endapo atarudi Clouds FM basi angependa atangaze kwenye kipindi cha Jahazi.
Post A Comment: