Diwani wa Gwarama Kakonko Kigoma amefunguka na kusema kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphery Polepole anatumia vijana mbalimbali kumshawishi ili akubaliane naye na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CHADEMA na kuthibitishwa na Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene imesema kuwa vijana hao wamekuwa wakihangaika sana kumshawishi diwyani huyo ili ahamie CCM na kumuahidi kuwa watafanya kila mbinu ili ashinde tena uchaguzi akiwa ndani ya CCM.

"Tangu juzi natafutwa eti nikubaliane na Ndugu Humphrey Pole pole ili nijiunge na Chama Cha Mapinduzi. Ndugu huyu alikuja Kakonko, wiki iliyopita na baadae akaenda Dodoma ila aliacha vijana wanaofanya biashara ya kununua madiwani Kakonko na wanazunguka, usiku na mchana wakitafuta madiwani wa upinzani, wamenipigia simu nyingi,nina Audio zao,wanaahidi kukupa stahiki zote,na wanasema wao wanahakikisha unashinda udiwani kwa gharama yoyote ile"

Diwani huyo aliendelea kusimulia kisa hicho na kusema kuwa kiongozi huyo alirudi tena jana Machi 11, 2018 kufuatilia maendeleo ya kazi yake hiyo aliyoiacha na kudai kuwa yeye hawezi kununuliwa.

"Sijawahi kuona biashara ya watu katika umri wangu, nimeiona sasa, tena safari hii anayetaka kununuliwa ni mimi, Mungu lehemu taifa lako. Pesa zimetengwa ili kumununua diwani wa Gwarama.

Wanunuaji wetu wanatumia gari ya wagonjwa kukata misere mtaani kutafuta diwani ambaye wao wanataka akihame chama kwa Kusema nimekubali utendaji kazi"
Mbali na hilo Diwani huyo ameweka wazi kuwa hali ya madiwani wa Kakonko ni mbaya kwani wanadai posho zao za mwaka mzima na kusema kuna wakati wanaendesha vikao bila hata kuwepo kwa maji ya kunywa kama njia ya kutaka kuwategesha.

"Kakonko ina hali mbaya ya Kiuchumi kiasi kwamba madiwani tunadai posho miezi 12 sasa. Tunakopesha vikao, hatunywi maji kwenye vikao, kuna roho zipo zimesubiri uombe maji ya kunywa halafu upewe na sumu ili udiwani ambao ni uwakilishi wa wananchi ukome kwa kukukatiza maisha ili chama kinachoitwa pendwa kishinde, ushindi wa chama hiki ni mpaka adui afe kama siyo kufanywa kilema kwanza"

"Nimewaambia viongozi wa dini biashara hii kama imefika Gwarama, nao wamesema nisikubali kuuza Uwakilishi huu kwasababu ya kutafuta urahisi wa maisha na chakula.Na mimi nilishakubali kuongozana na maskini wenzangu.

Naheshimu kura za maskini wenzangu, siwezi uza kura za hawa maskini wenzangu ili Mimi niutwae utajiri kwa kuwadhuru maskini." alisema diwani wa Gwarama
www.eatv.tv ilipomtafuta Katibu Mwenezi wa CCM, Humphery PolePole ili kujibu tuhuma hizo simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa
Share To:

msumbanews

Post A Comment: