Mwanamuziki wa Bongo fleva na CEO wa label ya WCB, Diamond Platnumz amefunguka na kusema kuwa chombo chochote cha habari ambacho kinaibania WCB kwa njia yoyote basi kitapotea kwani yeye ni kama maji usipokunywa utayaoga.
Diamond amekuwa mmoja wa wasanii ambaye amekuwa na migogoro na media mbali mbali ambapo siku za hivi karibuni Kumekuwa na sintofahamu kati yake na mkurugenzi wa Clouds Fm, Ruge Mutahaba.
Hii imekuja baada ya Diamond kutangaza kuanzisha stesheni zake za redio na Tv ambazo ni Wasafi Radio na Tv ambavyo amesisitiza vitacheza nafasi kubwa katika kukuza mziki wake na hata wasanii kutoka WCB kwa ujumla.
Diamond hivi sasa yuko nchini Kenya, Nairobi ambako ameenda kwenye uzinduzi wa albamu yake ya ‘A boy from Tandale’ ambayo inategemewa kuanza kuuzwa hivi karibuni.
Kwenye mahojiano na Dizzim Online, Diamond amefunguka kuhusu albamu yake ambayo ndani yake kuna nyimbo ambazo amewashirikisha wasanii kadhaa ikiwemo Rick Ross, Neyo na Omarion.
Lakini pia Diamond amefunguka kuhusu Wasafi Tv na Redio ambavyo vinategemea kuanza kuruka hewani siku za hivi karibuni lakini Diamond ameshangaa media zinazotaka kubania mziki wake kwani yeye ndio burudani yenyewe kwaiyo wao kumzuia yeye wanapotea:
"Yaani mimi nimejiwekea mazingira ambayo hata nikilala chumbani lazima utaniongelea huwezi kulala bila kunitaja aidha utawataja watoto wangu, au wasanii wa WCB au hata wapenzi wangu yaani Diamond ni kama Azam vile au mimi kama maji aidha utaninywa au utanioga yaani utajua mwenyewe lakini mimi huwezi kulala bila kunitaja kwaiyo media zinazozuia kazi zangu wanapoteza muda maana mimi ndio burudani na mzalisha burudani”.
Post A Comment: