Msanii wa muziki, Diamond Platnumz Ijumaa hii amefanya mazungumzo ya siri na Baraza la Sanaa Taifa ‘Basata’ ikiwa ni siku chache toka aingie kwenye majibizano na Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo “African Beauty” ametua viwanja vya basata majira ya nchana akiwa na meneja wake, Sallam SK. Hata hivyo baada ya kufanya mazungumzo hakuweza kuzungumza chochote juu ya nini kilitokea.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Basata zinadai muimbaji huyo alifika katika taasisi hiyo ya malezi ya wasanii kwaajili ya kuzungumza na viongozi hao juu ya kauli zake ambazo amekuwa akizitoa juu ya Naibu waziri huyo.
Hata hivyo Basata hawajatoa taarifa yoyote juu ya kikao hicho cha siri ambacho kilichukua masaa kadhaa.
Wadau wa mambo wanadai huwenda muimbaji huyo alikwenda Basata kwaajili ya kuamba radhi juu ya mambo yanayoendelea.
Mapema wiki hii muimbaji huyo wakati anahojiwa na kituo cha redio cha Times FM aliitupia lawama Basata pamoja na Naibu waziri huyo baada ya kufungia nyimbo 15 za wasanii wa bongofleva zikiwemo zake mbili.
Kauli hizo zilimfanya Waziri wa Habari, Dk Mwakyembe kutoa kauli yake na kudai kwamba ameshtushwa na kauli za muimbaji huyo juu ya waziri.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: