Ibrahim Ajibu.
WAPINZANI wa Yanga ka­tika Ligi ya Mabingwa Afrika, Township Rollers ya Bot­swana ni kama wamewakimbia Yanga baada ya kukimbilia nje ya mji.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa wa Botswana saa saba mchana kwa saa za huko sawa na saa nane mchana kwa Tanzania.
Obrey Chirwa
Katika mchezo huo, Yanga wataingia uwanjani na nyota wake walioisumbua safu ya ulinzi ya Rollers, Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu walioonyesha kiwango kikubwa katika mchezo huo.

Akizungumza na Championi  Hafidh Saleh alisema taarifa za kuondoka na kutimkia mji mwingine wamezipata kutoka kwa wenyeji wao ambao ni Watanzania waishio nchini humo wenye mapenzi na Yanga.

Saleh alisema kwa mu­jibu wa taarifa ambazo wamezipata wenyeji wao, walishangazwa na ujio wao wa mapema nchini hapa ambapo wameshtushwa na ujio huo wakihofia mbinu zao kujulikana, hivyo wakaona waondoke mjini hapo.

“Tangu tumefika hapa hatujawaona wapin­zani wetu Rollers zaidi tulipata taarifa za wao kukimbia mji kutukwepa sisi wakihofia kuzi­ona mbinu zao watakazozitumia.

“Hatujui wamekwenda kuweka kambi yao hiyo kwenye mji gani, kikubwa tunashukuru wenyeji wetu waliotupokea baadhi wak­iwemo Watanzania waishio hapa.

“Kingine tunafurahia mapokezi mazuri tu­liyoyapata kutoka kwa balozi wetu wa hapa nchini ambaye jana (juzi) tulikutana naye na kula chakula cha jioni na kubadilishana mawazo mbalimbali,” alisema Saleh.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: