Kurejeshwa kwa viwanja hivyo ni utekelezaji agizo la Mwenyekiti wa CCM taifa, rais John Magufuli alilolitoa hivi karuuni kwa kuunda tume ya kuhakiki maliz zote za CCM nchini.
Akizungumza mwishoni mwa wiki mwenyekiti wa CCM Kata ya Themi Thomas Munisi alisema viwanja vilivyorejeshwa ni pamoja na kilichokuwa eneo la relini karibu na kiwanda cha General Tyre pamoja na kiwanja kingine kilichokuwa nyuma ya ofisi ya CCM kata hiyo.
“CCM kata ya Themi tumejipanga kikamilifu kuhakikisha tunarejesha mali zetu zote zilizoporwa na baadhi ya viongozi waliokuwa na maslahi binafsi pamoja na watu wengine waliofanya CCM kuwa ni shamba la bibi kama mwenyekiti wetu wa CCM taifa alivyoelekeza kuwa mali zote za CCM zilizoporwa zirejeshwe mara moja”.
Kwa mujibu wa Munisi kiwanja kilichopo eneo la relini chenye thamani ya shilingi milioni 800 kilikuwa kimeporwa na mtu mmoja(hakumtaja jina) kwa miaka mingi lakini baada ya kukifuatilia tumebaini kuwa ni mali yetu na tumefanikiwa kurekirejesha.
Kuhusu kiwanja cha pili kilichopo nyuma ya ofisi hizo Munisi alisema kuwa baadhi ya wananhi wanaoishi jirani na ofisi ya CCM katika kata waliungana na kujimilikisha kiwanja hicho wakidai ni mali yao wanayomiliki kihalali lakini baada ya kufuata taratibu wamebaini kuwa ni mali ya CCM kata.
Munisi amewatuhumu baadhi ya viongozi waliopita kipindi cha nyuma kutumia madaraka yao vibaya kwa maslahi binafsi, kuuza na kufuja mali za chama bila woga wakati wakijua ni makosa kisheria .
“Kata ya Themi ni moja ya kata zenye miradi mikubwa katika wilaya ya Arusha lakini baadhi ya viongozi wazamani waliotutangulia walifuja mali zetu na kukifanya chama kushindwa kufanya shughuli za maendeleo katika kata hii kwa ajili ya kusaidia wanachama wake”
Aidha mwenyekiti huyo ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Arusha kuwahoji viongozi waliopita na kuhusia na na ubadhilifu wa mali za chama katika kata hiyo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Hatua hiyo imeungwa mkono na Umoja wa Vijana (UVCCM) katika kahiyo ambapo katibu wake Mathias Maico alisema kurejeshwa kwa viwanja hivyo kutakijengea chama imani kubwa kwa wananchi wa kata hiyo na kwamba wapo tayari kukisadia chama kupata mali zake.
“Nimpongeze mwenyekiti na viongozi wengine wa kata kwa juhudi walizozifanya za kurejesha viwanja hivi ambavyo vilikuwa vimeporwa hii itajenga imani kubwa kwa wananchi pamoja na vijana wenzangu abao sasa wameonyesha nia ya kurudi CCM
Post A Comment: