Katibu mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha Mjini Ndg. Abrahamu Joseph Mollel amemtaka Mbunge wa Arusha Godbless Lema kuacha siasa za maji taka kuhusiana na Madiwani walioamua kumuunga mkono Muheshimiwa Rais Magufuli.

Akizungumzaa na Msumbanews Blog Ndg. Abrahamu Mollel Amesema 
''Tunampa taarifa Lema kuwa Siasa za maandano na za porojo katika Mkoa wa Arusha hazina nafasi tena madiwani waliojizulu wameunga mkono utendaji wa  Rais Magufuli kwani ilani waliyokuwa wanaitekeleza ni ya Chama cha Mapinduzi hivyo waliona hawawezi kutekeleza majukumu yao nje ya Chama kilichopewa Ridhaa na wananchi ambacho ni CCM.''

Naye Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Wazazi Ndg. Victor Mollel Ameeleza kuwa 
''Lema atuachie mji wetu ukiwa salama na atafute kazi nyingine ya kufanya kama vile Kilimo na Mifugo ili tupate malighafi za viwanda kwani Arusha hawataki tena propaganda,Tunamshauri lema aje atuambie kwa miaka saba ya Ubunge wake amefanya nini mpaka sasa, Hivyo hao Madiwani  anaosema wameondoka kwa mafuriko awaache wamuunge mkono Rais wetu mpendwa Magufuli kwani yeye tutamrudisha kwa kimbunga.''

Hata hivyo Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM (M) Arusha Ndg. Omary Lumato amemalizia kwa kusema kuwa  ''Hii ndio gharama ya Demokrasia na ni salamu tosha kwa Lema pamoja na Meya Kalist Lazaro wajiandae kisaikolojia kukabidhi Jimbo la Arusha mjini 2020 pia watafute kazi nyingine za kufanya hata hivyo tunawatumia salamu wajiandae katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 kwani wananchi wanaimani na Serikali ya Awamu ya Tano.#Tukutanekazini.''
Share To:

msumbanews

Post A Comment: