Mtangazaji wa Clouds Tv, Casto Dickson amefunguka kuhusiana na uhusiano wake na Tunda Sebastian na kudai kuwa yupo tayari kumuoa na hajali kama ameshawahi kuchukuliwa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.
Siku za hivi karibuni uhusiano wa Tunda na Casto umetengeneza sana headlines Kwenye social media hasa kwa sababu Tunda alikuwa na urafiki na Muna ambaye ni mzazi mwenzake na Casto kwaiyo yeye kutembea na mwanaume wa rafiki yake ni kama unafki.
Mwezi uliopita ilisemekana kuwa Tunda ni mjamzito na Baba alitajwa kuwa ni Diamond lakini Casto amesema habari hizo sio za kweli kwani Tunda ana Kitambi kwa sababu anapenda kula ingawa anafanya mazoezi.
Casto amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Lemutuz Tv ambapo amekiri kuwa anampenda Tunda na yuko tayari kumuoa:
"Kuhusu Tunda kuwa na Diamond mimi hainisumbui wala hainihusu as long as tangu nimeenda kuwa naye I think kama mwezi na zaidi sasa tupo wenyewe na tunapendana na umri unaenda na maisha yanabadilika hivyo sidhani kama nina kosa kuweka wazi kuwa Nampenda Tunda na nina mpango wa kumuoa”.
Post A Comment: