Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii.

Sehemu iliyoathirika zaidi ni ile ya wauza mitumba huku baadhi ya bidhaa zao zikiteketea kwa moto lakini hakuna aliyeripotiwa kupoteza maisha wala kujeruhiwa.

Chanzo cha moto huo kinadhaniwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo tayari gari la jeshi la zima moto limefika  kuzima moto huo.
Taarifa zaidi tutakujuza

Share To:

msumbanews

Post A Comment: